Hapa naeleza hatari tunazoweza kuepuka ili simu yako iwe ni salama kwako na kwa wengine pia, hakikisha unaweka simu yako mbali na watoto au wanyama wa nyumbani. Kwanini jambo hilo ni la muhimu?
Sehemu fulani ni hatari ikiwa zitamezwa au zinaweza kutokeza mstuko utakao hatarisha uhai kwa mtoto au mnyama. Unaposikiliza simu hakikisha sauti ipo katika kiwango chenye kufaa, kwani ikiwa sauti imezidi kiwango cha kawaida inaweza kuleta tatizo kwenye usikivu wako.
Epuka kutumia simu huku unaendesha gari ili kupunguza aksidenti za barabarani na kukudhuru wewe au watu wengine. Zima simu/usitumie simu hasa unapokuwa katika Kituo cha kuongeza Mafuta, Gesi, Kemikali au Kimiminika chochote kinachoweza kuwaka au kulipuka kwakuwa aina fulani za Vimiminika viweza kulipuka kwa urahisi vinapokuwa jirani na vifaa kama simu za mkononi. Hakikisha unapoona eneo lenye alama hii chini ni vyema kuzingatia ili kuepuka hatari mapema.
Zingatia haya kwani uhai wako na jirani yako ni jambo muhimu sana na uwezi kuupata mahali popote duniani. Kumbuka simu ni kifaa kuzuri lakini pia chaweza kuwa kibaya ikiwa kitatumika bila kufuata taratibu zenye kufaa.