Tunapozungumza kuhusu fasheni hii inamaanisha mitindo ambayo hasa inaegemea katika maswala ya Nguo, Viatu, Utengenezaji wa nywele, kupamba mwili na vifaa vinavyotumika kwa kazi hizo au thamani za nyumbani, kama viti, meza, vitanda na n.k.
Fasheni inaweza kuwakilisha mtindo wa maisha wa watu katika mavazi, kujipamba n.k. Na neno fasheni pia hutumika katika bidhaa mpya zinazobuniwa kila siku na wabunifu wa mitindo. Leo kumekuwa na mitindo ya aina mbalimbali ya mavazi, mengine wala huwezi kutegemea kama litaweza kuvalia mahali fulani, na kumekuwa na watu maharufu duniani ambao kazi zao kubwa ni ubunifu wa mavazi ya aina mbalimbali, au Vifaa vya michezo na kieletroniki, kwa hapa Nyumbani Tanzania wapo pia kama akina Mustapha Assanary ambaye kazi yake kubwa ni ubunifu wa mavazi, na wenginee wengi.
Kwa ujumla mitindo ya mavazi au vitu, vimefanya kila kukicha watu wafikilie zaidi juu ya mambo hayo.
Unamaoni gani?