Chumba chenye kuvutia‼! Hakuna mtu asiyependa kuishi kwenye chumba chenye kuvutia.Lakini je,uliwahi kujiuliza ufanye nini ili chumba chako kivutie?
Yafuatayo ni madokezo machache ya jinsi ya kufanya chumba chako kuwa chenye kuvutia.
1.Tambua rangi ya kuta za chumba chako.Mapambo yote ya chumba lazima yaendane na rangi ya chumba chako.Tukisema mapambo tunamaanisha mapazia,mito,vitambaa vya makochi na meza,foronya za mito na hata maua.Kama ni chumba cha kulala basi pia mashuka yanahusika. Uchaguzi mzuri wa rangi za mapambo hayo zinazoendana vizuri na rangi ya kuta zako waweza kufanya chumba chako kuwa chenye kuvutia.
2.Epuka msongamano wa vitu. Hakikisha kila kitu kinakaa kwa nafasi na kuruhusu nafasi ya kutosha kupita bila kulazimika kogongana na vitu.Hiyo itafanya chumba kuwa chenye kuvutia na pia kuruhusu mzunguko mzuri wa hewa safi chumbani.
3.Kuwa mbunifu.Kuna njia tofauti tofauti za upangaji wa vitu unaoweza kufanya chumba chako kivutie.Tafuta vitu vya ziada kama vile mapambo ya ukutani.Mapambo haya si lazima yawe ya kununua dukani,unaweza ukabuni mwenyewe na hivyo kupunguza gharama.Unaweza kutengeneza mapambo hayo kutokana na vitu vya kawaida katika mazingira yako.
4.Taa.Taa pia zaweza kufanya chumba kuwa chenye kuvutia.Siku hizi kuna taa za miundo tofauti tofauti na mwanga tofauti pia.Chagua mwanga wa taa kufuatana na rangi za kuta zako.Kama chumba chako kina rangi angavu sana,ingekuwa vizuri kuchagua taa angavu kiasi ili kuepuka kuumiza macho.Kama chumba kina kuta zenye rangi za giza(zisizong’aa),ni vizuri kuchagua taa zenye mwanga mwangavu.
5.Zulia.Uchaguzi mzuri wa zulia waweza pia kufanya chumba chako kuwa chenye kuvutia.Chagua vizuri rangi na zingatia malighafi zilizitumika kutengenezea zulia hilo.
Ukizingatia hayo machache,chumba chako kitakuwa chenye kuvutia licha ya saizi yake(iwe ni kikubwa au kidogo).
Tukutane wakati ujao.Tchao‼‼!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni