Pole
uwenda ukashangaa kichwa cha habari cha makala hii hapo juu, lakini ndivyo hali
zilivyo. Watu wengi wanatumia vitambaa vya aina mbalimbali kama
vilivyotengenezwa na pamba au nailoni kwa ajili ya kukaushia vyombo vyetu vya
chakula baada ya kuviosha. Shughuli hizi hufanyika kila siku nyumbani au katika
mikahawa mbalimbali iwe mjini au pembezoni mwa miji.
Ni
jambo zuri kukausha vyombo baada ya kuvisafisha kwa sabuni na maji, na kuviacha
vikiwa vikavu na jambo hilo huepusha vyombo kufuatwa na bakteria wanaovutiwa na unyevunyevu wa maji kwa
urahisi na hivyo kuzaliana na mwisho kuleta hatari ya kupata magonjwa.
Kitambaa |
Uchunguzi
wa kisayansi umegundua kuwa vitambaa vinavyotumika kukaushia maji katika vyombo
vya chakula huwa na bakteria wengi zaidi ya wale wanaopatikana katika kinyesi.
Kwanini bakteria hao wapatikane katika
vitambaa hivyo?
Imeonekana
kuwa vitambaa hivyo baada ya kutumika vinasahaulika ama kuachwa vikiwa vimelowa
maji yaliondolewa katika vyombo, hivyo jambo hilo huvutia sana bacteria hao
wapendao unyevu, na wanapofanikiwa kuingia uzaliana kwa wingi na huendelea
kufurahia mazingira hayo. Mwisho wa siku wanaweza kusababisha magonjwa ya tumbo
na n.k.
Fikiria
kuwa ikiwa bakteria hao ni zaidi ya wanaopatikana katika kinyesi, je, basi
vyombo vyetu vitakuwa safi kadiri gani? Kwakuwa kila siku vinakaushwa na
vitambaa vilivyo katika hali hiyo.
Mambo
yafuatayo yanaweza kukusaidia kufanya Vitambaa vyako kuwa safi na salama na
hata kuepuka kuwa na bakteria hao hatari kwa afya zetu na hata wageni watakao
tutembelea.
- Hakikisha unapotoka
chooni unanawa mikono kwa sabuni na maji safi. Hilo ni jambo muhimu sana kwani
kutaepusha kuwaamisha bakteria hao kwenda katika vitambaa vya kukaushia vyombo.
Kunawa mikono kwa Sabuni na Maji safi. - Hakikisha baada ya kukitumia unaweka mahali ambapo kitakauka mapema zaidi.
- Hakikisha unakifua vizuri kitambaa kwa sabuni zenye Uwezo wa kuua bacteria na kusuuza kwa maji safi.
- Kitunze mahali salama na penye hewa ya kutosha, kwani unapoweka mahali pasipo wazi bakteria hawa ni rahisi kwao kuzaliana.
- Unapokifua, anika juani ili kuua bakteria.
- Kisafishe kitambaa angalau kila baada ya siku mbili ili kuendelea kuweka salama kitambaa chako dhidi ya bakteria.
- Baada ya kukuhakikisha kuwa kitambaa chako ni kikavu, kwa usalama zaidi kipige pasi.
Natumaini
habari hii itakusaidia kufanya mabadiliko jikoni kwako na kupafanya kuwa mahali
salama kwa afya.