Simu aina ya Xolo Q2000 imeingia sokoni ikiwa na kioo cha ukubwa wa 5.5” katika muundo wa Phablet. Ikitumia mfumo wa
Android 4.2 Jelly Bean na ikitumia
MediaTek Quad-core processor 1.2GB , RAM ya 4GB huku ikiwa na kitunza taarifa
cha ukubwa wa 8GB kilichojengwa ndani ya simu moja kwa moja.
Xolo Q2000 |
Pia inauwezo wa
kupachika kitunza taarifa cha ziada (Memory Card) cha hadi 32GB. Si hayo tu,
ina kamera yenye uwezo mkubwa wa 13 Megapixel na betri yenye 2600mAh yenye Uwezo
wa kukaa hadi masaa 17 hapa ina maana unaongea bila kukata simu. Na Saa 12
ikiwa unatumia mtandao wa Intaneti wa 3G.
Simu hii inapatikana kwa sasa katika
rangi Nyeusi tu kwa gharama ya $ 240 ambayo kwa pesa za hapa Bongo itakuwa Tsh.
384,000/= hivi.
Hiyo ndio Xolo Q2000 Toka china, Una maoni yoyote kuihusu?