Shughuli za UWEZO zinaendelea Mkoni Morogoro katika Manispaa ya Morogoro Mjini.
Baadhi ya wahojaji wakiwa katika vikundi vya majadiliano. |
Ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo kwa wahojaji wa kujitolea wakiwa wanapata mafunzo katika ukumbi wa shule ya msingi Leena iliyoko mkoani Morogoro, Kigurunyembe. Wahojaji wengi walifurahia namna mafunzo yalivyofanywa kwa muda huo wa siku mbili.
Wahojaji wakiwa makini wakimsikiliza Mkufunzi Bi. Shella Shomari hayupo pichani. |
Mambo kadha yalizungumziwa katika mafunzo hayo ya siku mbili kama:
Kuitambulisha uwezo, mchakato wa utafiti, mambo watakayo yafanya watakapotembeleza shule, kupima watoto uwezo wao wa kusoma na kufanya hesabu, namna wanavyoweza kufanya mrejesho wa papo kwa papo na masuala ya kimadili.
Wahojaji wakiwa wanajadili jambo wakati wa mafunzo hayo ya siku mbili.
|
Na walimu wa mafunzo hayo alikuwa Bi. Shella Shomari Mratibu Msidizi,Bi. Hellen Nkalang'ango ambaye pia ndiye Mratibu wa Wilaya katika masuala ya UWEZO na Bwa. Mahamud A. Ngamange.
Na shughuli za UWEZO zinafanyika katika Nchi 3 za Afrika Mashariki Tanzania, Uganda na Kenya.
Mafunzo yalikwisha vizuri na washiriki wakiwa tayari kunza kazi hiyo ya siku mbili, wakianzia kwa wenyeviti wa mitaa, shuleni na kisha siku ya tarehe 12 /10/2013 wataelekea katika Kaya mbalimbali kwa ajili ya mahoji.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni