Hapa kuna mambo uanayopaswa kuzingatia kabla ya kuamua kufanya hivyo
mapema kabla ya kununua simu iliyotumia kwa maneno mengine kwa lugha ya kigeni (Used
Phone).
Fuatana nami katika mfululizo huu wa ulimwengu wa sayansi na teknolojia nami
mwandishi wako Samuel Mwaleni wa makala hii.
Kwa kawaida watu wengi huamua kununua simu ambazo zimekwishatumika toka
kwa mtu Fulani. Kwanini? Lengo ni kuepuka gharama ya simu husika, huenda
kwakuwa simu hiyo dukani ni ghali sana au ni simu ulioipenda kwa muda mrefu na
hukufanikiwa kuipata kwakuwa ilikuwa ni ya gharama kubwa wakati huo, huenda
miaka 3 iliyopita.
Si vibaya kununua simu iliyokwishatumika toka kwa mtu fulani au hata
dukani kwakuwa wapo wenye maduka ambao huuza bidhaa zilizokwisha upya wake
maarufu kama mitumba. Ila waweza kuzingatia mambo yafuatayo kabla ya kununua
bidhaa hizo au simu hiyo uipendayo.
Si vibaya kununua simu iliyokwishatumika toka kwa mtu fulani au hata
dukani kwakuwa wapo wenye maduka ambao huuza bidhaa zilizokwisha upya wake
maarufu kama mitumba. Ila waweza kuzingatia mambo yafuatayo kabla ya kununua
bidhaa hizo au simu hiyo uipendayo.
Jambo muhimu kumbuka kuwa mwangalifu. Zaidi ya yote ni bora kununua
bidhaa ikiwa mpya kwakuwa bado kuna kampuni kubwa duniani zilizo na akiba ya
simu za toleo la zamani lakini bado zikiwa mpya kabisa. Kampuni kama ya Apple
bado inauza simu zake za Iphone 4S na Iphone 3gs na ikiwa
unahitaji unaweza kupata kwa gharama nafuu ukilinganisha na wakati zilipoingia
sokoni. Kampuni ya Samsung nayo ina simu zake za Samsung Galaxy S3 .
Na jambo la kukumbuka kuwa simu nyingi kama hizo juu huenda
utakapoinunua utakosa huduma mpya zinazongia sokoni kwa sasa kama iSO7 ambayo
ikiwa umenunua simu aina ya Iphone 3gs huwezi kuweka mfumo huo mpya kuendesha
simu yako kwa njia ya kisasa zaidi.
Kumbuka pia simu hutofautiana muundo, chunguza simu unayotaka kununua
ina muundo gani. Hii inamaanisha kuwa zipo simu ambazo unaponunua hutoweza
kuondoa betri yake ila tu umendaliwa sehemu maalumu unapoweza kuweka line yako
ya simu na kitunza data, muziki na picha. Aina nyingine hazikuundwa uweke kitunza
data, muziki na picha zako ila kitunza data kimeundwa moja kwa moja ndani ya
simu. Hivyo fikiria ikiwa ni ya muda mrefu, betri ikifa utafanya nini?
Kumbuka pia huwezi kubadili mfumo wa uendeshaji wa simu zinazotumia Android
OS, Window phone OS, ios au BlackBerry OS tofauti na vile watengenezaji
walivyozitengeza. Hivyo kabla ya kununua jiulize: baada ya kununua utahitaji
kubadilisha mfumo wake wa uendeshaji? Kumbuka ni jambo lisilowezekana hata kidogo.
Na ikiwa mfumo wa uendeshaji umepitwa na wakati na simu hiyo ni toleo la miaka
3 au 4 iliyopita kuna uwezekano mkubwa kutoweza kupata huduma mpya za kisasa
kwa simu hiyo kwani teknolojia inabadilika na kuwa ya kisasa siku baada ya
siku.
Nunua simu kwa gharama nafuu huku ukijua ni mpya na ni toleo la karibuni
angalau miaka 2 iliyopita hadi mwanzoni mwa mwaka huu.
Zipo simu za gharama nafuu na za kisasa kama Nexus 4 na Nokia Lumia 520,
Samsung Galaxy Star na Samsung Galaxy Pocket ambazo ni kama
160,000/= hadi 350,000/= kwa pesa za Tanzania.
Ushauri, ni bora ununue simu kwa gharama nafuu katika maduka
yanayoaminika na kupata warrant itakayokusaidia ikiwa simu uliyonunua inaleta
tatizo na itakuwa rahisi kuirudisha na kurekebishiwa au kubadilishwa na kupewa
nyingine. Ikiwa unanunua kwa mtu ni vyema kuifahamu simu hiyo na sababu ya yeye
kuiuza, ikibidi ingia katika tovuti ya simu husika kujua ina mambo gani yanayohusika.
Kwakuwa sasa kuna baadhi ya makampuni yamekuwa waigaji wazuri wa bidhaa za
kampuni nyingine kwa nia ya kunufaika kupitia jina la kampuni hizo.
Jua pia alinunua lini simu hiyo, itakuwa jambo zuri kama atakupatia
kitabu chake cha maelekezo ya matumizi ya simu hiyo.Baada ya hapo ndipo ufanye
uamuzi wa kununua au kutonunua simu hiyo.
Pia ni muhimu kujua uhalali wa bidhaa hiyo.Imekuwa kawaida leo kwa watu
kuiba simu madukani na kuziuza mtaani kwa bei nafuu.Hivyo chunguza kwa makini
ikiwa bidhaa hiyo si ya wizi.
Hayo ni mambo muhimu ya kuzingatia unaponunua bidhaa
zilizotumika.Tukutane wakati mwingine katika makala nyingine ya teknolojia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni