Translator

IMETOSHA

HHCTZ

BREAKING NEWS



BREAKING NEWS: Losam5 ....>>>>>>"Fashion,Entertainments,Science and Technology".......>>>>>>>Smile's Zone 5

Jumatano, 20 Novemba 2013

UNATAKA KUANZISHA BLOG?



Kila mtu huwenda akasema ndiyo. Watu wengi leo wamenzisha blog za aina mbalimbali kama za mitindo, michezo, burudani , za mashirika au za kibinafsi.

Je, wewe ungependa kuanzisha blog ya aina gani? Kwanini unataka kuanzisha blog? Je, blog yako italenga nini? 

Maswali hayo ya muhimu sana kabla ya kuamua kuanzisha blog yako. Utahitaji utafakari kwa kina ili ujue sababu za kutaka kuanzisha blog. Watu wengi ulimwenguni leo wamevutiwa na kuanzisha blog kwakuwa wataweza kuuelezea umma kwa njia rahisi kuhusu maisha yao, burudani au habari zinazojitokeza pembe mbalimbali za dunia. 

Hata hivyo wengine kwa kutojua ama kujua wameshindwa kuendelea kuendesha blog zao kwa kukosa jambo la kuandika na hilo hupelekea kufa kwa blog zao. Kwa uchunguzi wangu, inaonyesha wengi wao hawakujua kwanini waliamua kufungua blog, hivyo walijikuta wanashindwa kujua wanataka kufanya nini katika blog zao au wataandika nini.

Basi kabla ya kuamua kufungua blog kwanza tafakari maswali hayo juu. Yatakusaidia kufanya maamuzi sahihi kuwa blog unayohitaji kufungua itahusu nini au italenga nini. Hakikisha katika mipango yako, una uhakika wa kuandika makala zitakazoendana na blog yako. Mfano: kama blog yako inahusu burudani lakini wewe unaandika makala kuhusu ujenzi au uundaji wa ndege, hapo utamchanganya msomaji wako.

Hakikisha makala utakazoweka si zile za kukopi toka blog za watu wengine ambao wao waliumiza vichwa vyao na kutumia saa nyingi kuzitayarisha halafu wewe unaziamisha. Unapaswa kujikakamua kubuni makala zako ambazo wengine pia watavutiwa nazo.

Tuonane teka katika makala nyingine jinsi ya kujisari ili kuanzisha blog yako.