Kila
mtu huwenda akasema ndiyo. Watu wengi leo wamenzisha blog za aina mbalimbali
kama za mitindo, michezo, burudani , za mashirika au za kibinafsi.
Je,
wewe ungependa kuanzisha blog ya aina gani? Kwanini unataka kuanzisha blog? Je,
blog yako italenga nini?
Maswali
hayo ya muhimu sana kabla ya kuamua kuanzisha blog yako. Utahitaji utafakari
kwa kina ili ujue sababu za kutaka kuanzisha blog. Watu wengi ulimwenguni leo wamevutiwa
na kuanzisha blog kwakuwa wataweza kuuelezea umma kwa njia rahisi kuhusu maisha
yao, burudani au habari zinazojitokeza pembe mbalimbali za dunia.
Hata hivyo
wengine kwa kutojua ama kujua wameshindwa kuendelea kuendesha blog zao kwa
kukosa jambo la kuandika na hilo hupelekea kufa kwa blog zao. Kwa uchunguzi wangu,
inaonyesha wengi wao hawakujua kwanini waliamua kufungua blog, hivyo walijikuta
wanashindwa kujua wanataka kufanya nini katika blog zao au wataandika nini.
Basi
kabla ya kuamua kufungua blog kwanza tafakari maswali hayo juu. Yatakusaidia
kufanya maamuzi sahihi kuwa blog unayohitaji kufungua itahusu nini au italenga
nini. Hakikisha katika mipango yako, una uhakika wa kuandika makala zitakazoendana
na blog yako. Mfano: kama blog yako inahusu burudani lakini wewe unaandika makala
kuhusu ujenzi au uundaji wa ndege, hapo utamchanganya msomaji wako.
Hakikisha
makala utakazoweka si zile za kukopi toka blog za watu wengine ambao wao
waliumiza vichwa vyao na kutumia saa nyingi kuzitayarisha halafu wewe
unaziamisha. Unapaswa kujikakamua kubuni makala zako ambazo wengine pia
watavutiwa nazo.
Tuonane
teka katika makala nyingine jinsi ya kujisari ili kuanzisha blog yako.