Translator

IMETOSHA

HHCTZ

BREAKING NEWS



BREAKING NEWS: Losam5 ....>>>>>>"Fashion,Entertainments,Science and Technology".......>>>>>>>Smile's Zone 5

Jumatano, 20 Novemba 2013

JE, WAJUA KUWA KITAMBAA CHA KUKAUSHIA VYOMBO KINAWEZA KUWA NA BAKTERIA WENGI ZAIDI KULIKO WALE WANAOPATIKANA KATIKA KINYESI?

Pole uwenda ukashangaa kichwa cha habari cha makala hii hapo juu, lakini ndivyo hali zilivyo. Watu wengi wanatumia vitambaa vya aina mbalimbali kama vilivyotengenezwa na pamba au nailoni kwa ajili ya kukaushia vyombo vyetu vya chakula baada ya kuviosha. Shughuli hizi hufanyika kila siku nyumbani au katika mikahawa mbalimbali iwe mjini au pembezoni mwa miji.

Ni jambo zuri kukausha vyombo baada ya kuvisafisha kwa sabuni na maji, na kuviacha vikiwa vikavu na jambo hilo huepusha vyombo kufuatwa na bakteria  wanaovutiwa na unyevunyevu wa maji kwa urahisi na hivyo kuzaliana na mwisho kuleta hatari ya kupata magonjwa. 

losam5
Kitambaa
Uchunguzi wa kisayansi umegundua kuwa vitambaa vinavyotumika kukaushia maji katika vyombo vya chakula huwa na bakteria wengi zaidi ya wale wanaopatikana katika kinyesi. Kwanini  bakteria hao wapatikane katika vitambaa hivyo? 

Imeonekana kuwa vitambaa hivyo baada ya kutumika vinasahaulika ama kuachwa vikiwa vimelowa maji yaliondolewa katika vyombo, hivyo jambo hilo huvutia sana bacteria hao wapendao unyevu, na wanapofanikiwa kuingia uzaliana kwa wingi na huendelea kufurahia mazingira hayo. Mwisho wa siku wanaweza kusababisha magonjwa ya tumbo na n.k. 

Fikiria kuwa ikiwa bakteria hao ni zaidi ya wanaopatikana katika kinyesi, je, basi vyombo vyetu vitakuwa safi kadiri gani? Kwakuwa kila siku vinakaushwa na vitambaa vilivyo katika hali hiyo.
Mambo yafuatayo yanaweza kukusaidia kufanya Vitambaa vyako kuwa safi na salama na hata kuepuka kuwa na bakteria hao hatari kwa afya zetu na hata wageni watakao tutembelea.

  1.  Hakikisha unapotoka chooni unanawa mikono kwa sabuni na maji safi. Hilo ni jambo muhimu sana kwani kutaepusha kuwaamisha bakteria hao kwenda katika vitambaa vya kukaushia vyombo.   
    losam5
    Kunawa mikono kwa Sabuni na Maji safi.
  2.  Hakikisha baada ya kukitumia unaweka mahali ambapo kitakauka mapema zaidi.
  3. Hakikisha unakifua vizuri kitambaa kwa sabuni zenye Uwezo wa kuua bacteria na kusuuza kwa maji safi.
  4. Kitunze mahali salama na penye hewa ya kutosha, kwani unapoweka mahali pasipo wazi bakteria hawa ni rahisi kwao kuzaliana. 
  5.  Unapokifua, anika juani ili kuua bakteria.
  6. Kisafishe kitambaa angalau kila baada ya siku mbili ili kuendelea kuweka salama kitambaa chako dhidi ya bakteria.  
  7.  Baada ya kukuhakikisha kuwa kitambaa chako ni kikavu, kwa usalama zaidi kipige pasi.
Natumaini habari hii itakusaidia kufanya mabadiliko jikoni kwako na kupafanya kuwa mahali salama kwa afya.