Translator

IMETOSHA

HHCTZ

BREAKING NEWS



BREAKING NEWS: Losam5 ....>>>>>>"Fashion,Entertainments,Science and Technology".......>>>>>>>Smile's Zone 5

Jumamosi, 26 Oktoba 2013

KUGEUZA TAKATAKA KUWA KITU CHENYE FAIDA

Waweza kushangaa takataka inawezaje kuwa faida. Kuna vitu vingi ambavyo tunaviona kuwa takataka lakini vyaweza kugeuzwa kuwa vitu vyenye faida kwetu.
losam5
Baadhi ya Takataka
 
Takakata hizo zaweza kutumika kutengeneza vitu tofauti touti kama Opener, Kadi, Bangili, Heleni, Taa, Urembo wa ukutani na hata kuwa vyombo vya kurembea.
 
Fikiria vitu vichache vifuatavyo ambavyo vyaweza kuwa faida kutoka kwenye takataka.
 
1. Vifuu vya nazi
Wengi baada ya kutumia nazi, vifuu tunavitupa. Lakini vifuu hivi vyaweza kutumika kutengeza taa au hata hereni, bangili na vibanio vya nywele.
 
2. Kalenda zilizokwisha
Kalenda pia zaweza kutumika kutengeza taa au hata urembo wa ukutani. Pia zaweza kutumika kujaladia daftari au vitabu ili visichafuke na hivyo kudumu muda mrefu.
losam5
Karenda zilizokwisha muda wake kama hizi zaweza kuwa faida
 
3. Mbegu za Miti
Baadhi ya mbegu hutumika kaa urembo kwaajili ya kupambia nguo. Zinatumika kama zinavyotumika shanga katika kuremba nguo. Pia hutumika kutngeza mikufu na vidani au hata hereni.
 
4. CD zilizotumika
Hizi pia zaweza kutumika kutengeza urembo wa ukutani. Pia zaweza kutumika kutengeza maua  mauwa na kadi.
losam5
Takataka za CD's kama hizi zinaweza kuwa faida kwako
 
5. Chuma za Maji
Chupa za maji zawza kutumika katika utengenezaji wa taa, kifaa cha kuweka vidani au hata maua.
 
6. Vifuniko vya Chupa za Soda au Maji
Hivi ni vizuri sana katika kutengeneza vikapu au kutumika kama urembo wa vikapu. Pia vyaweza kutumika kama malighafi katika kutengeneza maumbo tofauti tofauti kwaajili ya urembo wa ukutani.
 
7. Vijiiti au Miti iliyokauka
Hii pia yaweza kutumika badala ya maua. Ubunifu unahitajika unapoviandaa ili kuvitumis kama urembo wa ndani. Waweza kuviweka kwenye vyungu vikubwa au vidigi na hivyo kupendezesha chumba.
 
Baada ya kukupa hayo mawazo machache, fikiria jinsi ya kugeuza takataka nyingine kuwa vitu vyenye faida bila kutumia gharama.
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni