Translator

IMETOSHA

HHCTZ

BREAKING NEWS



BREAKING NEWS: Losam5 ....>>>>>>"Fashion,Entertainments,Science and Technology".......>>>>>>>Smile's Zone 5

Alhamisi, 11 Novemba 2010

ENZI ZA UVUMBUZI WA INJINI

Karl Benz
Mvumbuzi wa injini ya petrol
Magari maarufu duniani Mercedes Benz yanatokana na jina la Huyu Mjerumani Karl Benz, ambaye alizaliwa 1844 huko Muhlburg.
Ni karl Friedrich Benz, amabaye alishirikiana na Wajerumani wengine kama Gottlieb Daimler katika kuvumbua kile kilichokuja kuitwa Injini….ambapo Benz alipata atimiliki kwakuwa hasa yeye alikuwa mvumbuzi wa Injini hiyo mnamo mwaka 1886 akiwa na umri wa miaka 42.
Huyu karl Benz baba yake alikuwa ni dereva wa gari moshi (Treni), na alipokuwa na umri wa miaka miwili baba yake alikufa, hivyo baada ya baba yake kufa aliamua kubadili jina lake na kujiita jina la baba yake kama kumbukumbu ya baba yake.
Kilichomsukukuma kuamua kufikia ubuni wa Injini , ni kuchoshwa na safari zenye kuchosha za kila siku kwa kutumia miguu, hivyo alitamani kupata kitu kitakachorahisisha safari hizo…ambacho hakitamfanya mtu atumie nguvu nyingi katika safari yake, hivyo alitengeza kifaa kinachomia magurudumu manne na akaiwekea injini iliyotumia Mvuke wa maji moto na usafiri huo akaupa jina la Benz Patent Motorwagen. Bwana Karl Benz alikufa akiwa na umri wa miaka 84.
Huo ukawa mwanzo wa uvumbuzi wa Injini za Petrol Duniani, hivyo leo kampuni kubwa ya Magari ya Mercdes Benz imetegea sana uvumbuzi wa huyu mtu na inaendelea kumuasisi Bwana Karl Benz.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni