Translator

IMETOSHA

HHCTZ

BREAKING NEWS



BREAKING NEWS: Losam5 ....>>>>>>"Fashion,Entertainments,Science and Technology".......>>>>>>>Smile's Zone 5

Jumamosi, 9 Novemba 2013

TEKNOLOJIA YA HABARI NI NINI?

Ni "utafiti, urasimu, uendeleshaji, utekelezaji, usaidizi au usimamizi wa mifumo ya habari hasa ala za programu na vifaa vya kompyuta."  IT inahusika na matumizi ya kompyuta zitumiazo umeme na programu za kompyuta kuzibadili, kuhifadhi, kulinda, kuchecheta, kueneza, nausalama katika kupokea habari.

Leo, neno habari limezunguka nyanja nyingi za kompyuta na teknolojia, na neno hili limekuwa maarufu sana Ulimwenguni. Wataalamu wa IT hutekeleza majukumu mbalimbali kutoka kuweka ala hadi kubuni mitandao tata ya kompyuta na hifadhidata za hali ya juu. Machache kati ya wajibu ya wataalamu wa IT ni kufanya usimamizi wa data, kujumuisha kompyuta ili kutengeneza mtandao, uhandisi wa hifadhidata na programu na vilevile usimamizi na utawala wa mfumo mzima.

Wakati kompyuta na teknolojia za mawasiliano zinapounganishwa, matokeo ni teknolojia ya habari, au "infotech". Teknolojia ya habari ni neno la jumla linaloelezea teknolojia yoyote ambayo husaidia katika kuzalisha, kuendesha, kuhifadhi, kuwasilisha, na / au kusambaza habari. Kwa makadirio, wakati tunapozungumza kuhusu teknolojia ya habari (IT) kwa ujumla, ni uthibitisha kuwa matumizi ya kompyuta na habari yanashirikiana kwa kila nyanja.